Jumanne, 18 Agosti 2015

AHADI YA UADILIFU ITAIMARISHA MAADILI YA KIBIASHARA,HUDUMA ZA JAMII




TUESDAY, AUGUST 18, 2015

Ahadi ya Uadilifu itaimarisha maadili ya kibiashara, huduma kwa umma.

Na Mwandishi Wetu 

“Suala la maadili si jipya, Watanzania watakumbuka tangu enzi la Azimio la Arusha misingi ya maadili imekuwa ikisisitizwa kama kijenzi muhimu cha ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma,” ni kauli ya Tixon Nzunda, Naibu Kamishna wa Maadili aliyoitoa siku ya uzinduzi wa Ahadi ya Uadilifu, Agosti 14, 2015, Ikulu Dar es Salaam. 

Kauli hii inasadifu ninachotaka kukieleza hapa katika makala haya na kwa hakika kumpa kongole Rais anayemaliza muda wake, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kuhuisha suala la maadili kama kijenzi muhimu cha ufanisi katika utendaji wa sekta za umma na binafsi. 

Itakumbukwa kuwa Ijumaa iliyopita Reais Kikwete alizindua kile kinachoitwa Ahadi ya Uadilifu ambapo viongozi kadhaa wa umma na kutoka sekta binafsi walitia saini hadharani ahadi za kuendesha shughuli zao kimaadili zaidi. 

Ahadi ya Uadilifu kimsingi ni tamko rasmi na bayana la dhamira ya kuwa na mwenendo wa kimaadili na kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Maadili na Mapambano dhidi ya Rushwa. Kwa kusaini tamko hilo mhusika au taasisi inakuwa vimejipambanua kwa umma kuwa hawatajiingiza katika masuala yasiyo ya kimaadili katika utoaji wa huduma na uzalishaji.

Wazo la kuwa na Ahadi ya Uadilifu ni ubunifu kutoka maabara ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) iliyokuwa ikiangalia mbinu za kuboresha sekta ya mazingira ya biashara nchini. 
Kwa mujibu wa wataalamu kutoka sekta za umma na binafsi waliokusanyika katika kufanya uchambuzi huo, ilionekana dhahiri kuwa rushwa bado ni tatizo katika uendeshaji wa shughuli za umma na binafsi.  

Pamoja na kuwepo sheria, kanuni, miongozo na mikakati ya kukuza maadili na kupambana na rushwa bado matokeo ya kuridhisha hasa katika kuinua utendaji na maadili katika uendeshaji wa biashara yavikupatikana. 
Wananchi bado wanalalamika kuwepo kwa urasimu usio wa lazima wenye lengo la kutengeneza mazingira ya rushwa na huduma zisizoridhisha katika utumishi wa umma. Wafanyabishara binafsi nao wapo baadhi hawana maadili na hata kufikia hatua ya kuchochea utoajiwa rushwa au kuzalisha bidhaa zisizo na viwango. 

Vile vile Sekta Binafsi haijashirikishwa vya kutosha katika Mkakati wa Kupambana na Rushwa na utamaduni umekuwa ni watu kuamini kuwa Rushwa iko katika sekta ya umma tu wakati wanaotoa rushwa kubwa wako katika Sekta Binafsi. 
Ni dhahiri kuwa Sheria, Kanuni, Miongozo na Mikakati iliyopo pekee haiwezi kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la rushwa na maadili. Hivyo kuhitaji mkakati wa ziada ambao utajenga mwitikio na dhamira kwa viongozi wa umma na kuishirikisha Sekta Binafsi katika mapambano dhidi ya rushwa na utovu wa maadili.

Hivyo kusainiwa kwa tamko la ahadi ya uaminifu kutasaidia kukuza maadili na kupambana na vitendo vya rushwa katika sekta ya umma na binafsi; ahadi au tamko hili linashawishi viongozi, watumishi wa umma na makampuni binafsi kuwa tayari kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadili na kupambana na rushwa kwa hiari yao wenyewe.

Katika tamko hilo kunawekwa kauli thabiti ya kimaadili ambayo inaonesha nia ya kufanyabiashara au kutekeleza majukumu ya umma kwa uadilifu na inakumbushwa Makampuni, Viongozi na Watumishi wa Umma juu ya wajibu wao wa kuzingatia Kanuni za Maadili na Mapambano dhidi ya rushwa. 

Misingi ya tamko hili imebebwa katika kukuza Uwazi, Uadilifu, Uwajibikaji na Utaalamu katika uendeshaji shughuli za umma; Kukuza mwitikio wa kupambana na rushwa kwa kuimarisha taratibu za udhibiti wa ndani. 

Misingi mingine ni pamoja na kusimamia masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma, na Kanuni za Maadili ya Kitaaluma; 
Pia ipo hoja ya kuimarisha mahusiano ya viongozi wa umma, watumishi wa umma au wamiliki na watendaji wa makampuni na wananchi au wateja wengine; Kudhibiti vitendo vya utovu wa maadili mahali pa kazi na kukuza uzalendo.  

Ili kufikia malengo ya ahadi hii Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Miradi (PDB) inayoratibu BRN ndiye mwangalizi mkuu wa kuona suala hili linaleta tija katika kufikiwa malengo mapana ya BRN.

Hata hivyo Sekretarieti ya Maadili ndiyo imepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa kila siku wa ahadi hizi ambapo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma itakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma kwa kuwashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Ili kuhakikisha utekelezaji unakuwa wa mafanikio kwa upande wa sekta binafsi Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) itakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Makampuni binafsi.

Inategemewa kuwa utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu utajenga mwitikio na dhamira ya uadilifu, uwazi, uwajibikaji, ari ya kupambana na rushwa na utoaji wa huduma bora katika Sekta ya Umma na Binafsi. 

Pia, utahamasisha Viongozi, Watumishi wa Umma na kuzingatia misingi ya maadili na Mapambano dhidi ya Rushwa. Aidha, kuwashirikisha wananchi kufuatilia vitendo vya utovu wa maadili miongoni mwa Watumishi wa Umma, Viongozi wa Umma na Sekta Binafsi na kutoa taarifa kwa mamlaka husika. 

Kwa namna hii hususani katika eneo la utoaji wa huduma na uzalishaji wa bidhaa watanzania watarajie kuimarika sana kwa uadilifu katika utendaji wa wahusika na kusaidia kufikia malengo ya BRN.

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, TPB KWA KUSHIRIKIANA NA PROPERTY INTERNATIONAL LIMITED WAZINDUA MPANGO WA KUWAKOPESHA VIWANJA WANACHAMA WA MFUKO HUO

 WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.
 Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake
 Msanii wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
 Mh. Samia Suluhu Hassa, akimpongeza Silayo baada ya kutoa hotuba yake. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi,(kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Abdulkarim Haleem.

NA K-VIS MEDIA
 MFUKO wa wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na  Benki ya Posta Tanzania, TPB, na Taasisi ya Property International Ltd leo Agosti 18, 2015 wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Hyatt Regency.

Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya  Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote.

 Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.

Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu. 

Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi  na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzia Maisha kwa wanachama wapya.

 Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.

Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.
 Mgeni Rasmi, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF.
 Mgeni rasmi, Samia, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPB.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PIL.
Moshingi, (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa PIL Zohra Moore, (kulia)
 Mh. Samia, (kulia), akisindikizwa na Silayo, wakati akiondoka ukumbi wa Hotel ya Hyatt, baada ya hafla hiyo.
Moshingi (kulia), akisalimiana na Mh. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.

UZINDUZI WA MRADI WA MAJI NA KITUO CHA MAENDELEO YA VIJANA

al4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifunguaMfereji ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katikaviwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja (katikati) Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hamad Yusuf Masauni.
al5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha ndoo ya maji Fathiya Khamis Husein (Suza)baada ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja.

al1

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja leo alipofika kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni
al2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua  Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika  Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja,(kutoka kushoto) Nd,Abdalla Suleiman  Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hmad Yusuf Masauni.
al3
Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji ZAWA wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja
al6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo wakati alipotembelea mabanda ya maeonesho ya kazi mbali mbali katika kituo cha Maendeleo ya Vijana Mwembe madema leo akiwa katika ziara ya kuzindua Mradi wa Maji na Kituo hicho katika Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
al7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) Nd,Abdalla Suleiman  (kulia)wakati alipotembelea kituo hicho Mwembe Madema kuona maendeleoya kazi mbali mbali zinazofanywa na vijana wa Jimbo la Kikwajuni  sambamba na uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama katika Jimbo hilo leo.
al8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinalipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema Jimbo la Kikwajuni leo.
al9
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi Jimbo la Kikwajuni samba mba na  Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema leo. 

TAMASHA LA MICHEZO LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 29

..Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade  Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la  10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.
 
habari na libeneke la kaskazini blog
Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.



Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.



"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema



Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.


Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel 

Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.



Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.



Tamasha hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega Trade,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini (NHC) Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi ya FAIDIKA na Tanzanite One.


Makamu Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Adrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa Tamasha hilo watatangazwa karibuni sambamba na zawadi na mgeni rasmi.

 Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari, ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Makamu Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea  vikombe kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace Hotel  kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo litashirikisha pia wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Wadhamini na viongozi wa TASWA Arusha, wakiwa kwenye kikao na waandishi wa habari kuelezea Bonanza la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha,ambalo litafanyika Augosti 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Dk Massaburi afurahia kuanza kwa huduma ya mabasi ya DART jijini Dar es salaam

HATUA ya kuzinduliwa kwa mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam, kumetibua mpango wa vyama vya upinzani, kumchafua mgombea wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Didas Masaburi na chama hicho.
Dk Masaburi ndiye Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kilichoundwa na serikali kusimamia mradi huo kukamilika haraka iwezekanavyo ili kuboresha usafirishaji wa abiria katika Jiji la Dar es Salaam na kukuza uchumi, Ubungo ikiwa ni mlengwa mkubwa kutokana na kuwekwa katika awamu ya kwanza ya mradi.
Habari za kuaminika zinasema baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walikusudia kutumia hoja za Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (DART), ubinafsishwaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na madai ya kutotumia nafasi ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam katika kuinufaisha Ubungo kama silaha za kumhujumu Dk Massaburi na CCM.
Baada ya Mradi wa DART  kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia jana, ukiwa chini ya waendeshaji wazawa, Kampuni ya UDA-RT ambayo inaundwa na wawekezaji wazawa Kampuni ya UDA na Muungano wa Wamiliki wa Daladala, hoja hiyo imepoteza nguvu.
Wakizungumza katika vijiwe maarufu vya upinzani vya Kosovo  na Sweet Corner vilivyopo Manzese jijini Dar es Salaam, wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliahidi kuzitumia hoja hizo ili kumdhoofisha Dk Masaburi wakati kampeni zitakapoanza.
Abbas Mwaimu wa CUF na Zebedayo Ngogo walisema wamejipanga kumuuliza Dk Masaburi maswali kuhusiana na hoja hizo, akisema mradi wa DART na UDA ni miradi hewa na isiyo na manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam, hususani Ubungo.
Kuzinduliwa kwa mabasi ya DART katika awamu ya kwanza ya utoaji wa mafunzo kwa madereva jana, kunawafanya wananchi na wajasiriamali wa Ubungo kilipo kituo kikubwa cha mabasi hayo kufikia  ndoto yao ya kupata ajira hasa kwa vijana na  upatikanaji wa ajira kwa vijana, ukuaji wa biashara kwa mamalishe na makundi mengine ya kijamii kutimia.
Kwa wakati tofauti jana, Waziri Ghasia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Dadiki, walisema Dk Masaburi akiwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kilichoundwa ili kusimamia Mradi wa DART kukamilika haraka, amefanya kazi kubwa inayoonesha jinsi Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli inawajali wananchi wake.
Mbali ya Mradi wa DART, Ubungo pia itanufaika na Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) ambapo Benki ya Dunia tayari imetoa Sh bilioni 8.76 ili kuboresha mazingira ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mpango huo, huku maeneo mbalimbali yakitegemewa kuboreshwa ikiwemo upanuzi na urekebishaji wa madaraja ya Mto Mbokomu ambao ni kero kwa wakazi wa Manzese.
Akizungumza kwenye uzinduzi jana, Dk Massaburi alisema; “Hayawi hayawi yamekuwa. Kinachofanyika leo kinadhihirisha namna serikali ya Rais Kikwete na Waziri Magufuli inavyowajali wananchi wake.
“Kuna watu walihaha ili kuhakikisha kuwa mradi huu wasipewe wazalendo wapewe wageni, lakini Rais Kikwete na Waziri Magufuli walisimama kidete. Waliokuwa wanabeza leo wanatakiwa kuzomewa bila kupepesa macho maana hatimaye mabasi yamefika.
“Mradi huu ni muhimu sana kwani utasaidia kuinua ajira, kipato, kuondoa umasikini kwa kuinua uchumi wa wajasiriamali, maana mahala inakopita barabara, viwanja vitapanda bei, vijana watapata ajira, na mama lishe watauza bidhaa mbalimbali. Lakini pia wageni watapenda kutumia usafiri huu kwa hiyo utalii ndani ya Dar es Salaam utakua,” alisema Dk Masaburi.
Aidha Dk Masaburi alitumia nafasi hiyo kuzitaka mamlaka husika kuwapa umuhimu wa pekee watu wanaoishi katika maeneo ya mradi wanapotoa ajira, huku akisema ni lazima wananchi wa Jimbo la Ubungo wapewe umuhimu wa nafasi za ajira.

EWURA FAMILY DAY ILIVYOFANA DAR

 Watoto wa familia za wafanyakazi wa wakishindana kukimbiaMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao (Ewura Family Day) kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Ewura wakiwa katika picha ya pamoja na familia zao
 Wakiwa katika mchezo wa Wavu
 Wakishindana kukimbia huku wakiwa kwenye magunia
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (kulia) akishiriki na wakurugenzi wenzie kushindana kuvuta kamba na wafanyakazi wa Ewura wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam juzi
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa siku ya kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (wa tatu kushoto) akishiriki kucheza mpira wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Waliovaa fulana za bluu wakishindana soka na waliovaa njano


 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo (kulia) akishiriki na wenzie katika shindano la kukimbiza kuku
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi akifurahia zawadi ya kuku aliyemkamata katika shindano la kufukuza kuku wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam juzi.



 Mwanafunzi Charles Daud ambaye ni mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Ewura akishangilia baada ya kushinda shindano la kufukuza kuku
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi kikombe kwa mmoja wa washindi wa michezo iliyofanyika siku hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi (kulia) akipokea kikombe kwa niaba ya wakurugenzi walioshinda katika mchezo wa kuvuta kamba
 Ngamlagosi akifurahia zawadi hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa nahodha wa timu ya ilivaa fulana ya njano  iliyoishinda  ya bluu katika shindano la kuvuta kamba
 Wafanyakazi na familia zao waliovaa fulana ya njano wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe hicho
 Mfanyakazi wa Ewura Rachel Kiula akifurahia kupata zawadi ya kikombe aliyopata baada ya mfanyakazi pekee aliyeshiriki katika michezo mingi iliyochezwa siku hiyo.
 Baadhi ya washindi wa michezo mbalimbali wakishangilia huku wakiwa na zawadi zao


 Sasa ni wakati wa msosi




 Kijana mchekeshaji Comedian akiwa kazini baada ya watu kupata msosi
 Sasa ni wakati wa watoto kufurahi




 Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakipata ushauri nasaha kuhusu masuala ya kulinda  afya zao
Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakiwa katika picha ya pamoja

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni