CCM
YATANGAZA KAMATI YA KUMWANGAMIZA LOWASA.
Dar
es salaam
Agost 18.2015
Ikiwa
zimebaki siku tatu filimbi ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu kuanza ambapo ni
Agost 22 mwaka huu,Chama cha Mapinduzi kimetangaza rasmi wajumbe wa kamati ya
kampeni ya kitaifa yya chama hicho.
Akitangaza kamati
hiyo leo katibu wa halmashauri kuu ya TAIFA,Itikadi na Uenezi Nape Mnauye
amesema kuwa kamati hiyo itakua na wajumbe 32 ambao wataongozwa na mwenyekiti
wa kamati hiyo Abdulrahman Kinana, makamu mwenyekiti bara Rajabu Luhwavi na
makamu mwenyekiti Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Wajumbe
wengine ni Sofia Simba,Mohamed Seif Khatib,Asha Rose Migiro,Samweli Sitta,Nape
Mnauye,Mwigulu Nchemba,Harrisoni Mwakyembe,January Makamba,Amina Makillagi,Christpher
Ole Sendeka,Stephen Wasira, Abdallah Bullembo,Hadija Aboud,Mohamed Aboud,Lazaro
Nyalandu,Issa Haji Ussi,Waride Bakari Jabu.
Wengine ni
Mohamoud Thabit Kombo,Shamsi Vuai Nahodha,Maua Daftari,Stephen Masele,Pindi
Chana,Shaka Shaka,Makongoro Nyerere,Benard Membe,Sadifa Juma Khamisi,Anthony
Diallo,Livingston Lusinde pamoja na Ummy Mwalimu.
KUVULIWA WADHIFA NDANI YA CHAMA.
Hivi
karibuni kuna taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Nape
Mnauye anavuliwa wadhifa wake huo kwa kile kinachodaiwa anaenda kinyume na
maadili ya kazi hiyo,hata hivyo amekanusha nakusema kuwa nitaarifa zisizo na
ukweli ndani yake .
“Sijajua
hata mimi kwanini taarifa hizi zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii,lakini
siyo mimi peke yangu ambaye nimesambaziwa taarifa za nammna hii,nadhani ni
dalili mbaya za ukawa ,injini yao inatoa moshi sana na hii ni kutokana na
kuchukua oili chafu(Lowasa) ”.alisema Mnauye.
USHINDI NDANI YA CCM.
Kuhusu
ushindi wa Uchaguzi Mnauye amesema
kuwa CCM itashinda kwa kishindo
kutokana na Mgombea wa Urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi Ukawa ambaye pia ni waziri wa
mstaafu Edward Lowasa kuwa na kashfa
za ubadhilifu wa fedha ikiwemo Richmond.
“Ukijua tekniki
za vita na anayeongoza ni komredi kinana ni mtaalamu wa stretejia za vita
subirini mapigo yake,nando maana taunasema tutampiga asubuhi tu,na nafikiri
siku hiyo ya uchaguzi nivizuri ambulance mbili zisogezwe kwake kwasababu baala
atakayoipa hatasahau maishani mwake,huwezi kuchukua fisadi mwizi na
aliyekataliwa na Mwalimu Nyerere.”alisema.
Kuhusu
ratiba ya uzinduzi wa kampeni ya CCM katibu huyo mwenerzi amesema ratiba
itatangazwa muda wowote baada ya mambo kukamilika .
Kamati kuu
ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa imefanya kikao chake cha
siku moja Agost 17 katika Ofisi zake Ndogo za zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Chini ya
Mwenyekiti wake Rais Dokta Jakaya
Kikwete na kuteuwa wagombea ubunge majimbo mawili ya Singida Mashariki na
Kiteto.
Walioteuliwa
kupeperusha bendera kwenye majimbo hayo ni Jonathan Njau(Singida Mashariki) na Emmanueli Papian Jonh(Kiteto) ambapo pia
hapo jana majimbo yapatao 9 yametangazwa.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni