IDADI YA WAGONJWA WALIYORIPOTIWA
KUAMBUKIZWA NA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU AMBAO UMELIKUMBA JIJI LA DAR ES
SALAAM PAMOJA NA MKOA WA MOROGORO IMEFIKIA WAGONJWA 262 NA VIFO 8….
Dar es salaam
Agost 25.2015
Idadi ya
wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao umelikumba
jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia wagonjwa 262,huku
vifo hadi sasa toka ugonjwa huo
ugundulike Agost 15 mwaka huu vikifikia nane.
Taarifa hiyo
imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif Rashidi wakati
akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa taarifa juu ya Ugonjwa
huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani
Morogoro.
Aidha alisema
kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam walioambukizwa ni
230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya
Kinondoni ina wagonjwa 186,Manispaa
ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba wagonjwa waliyolazwa kwenye
kambi za matibabu ni 71 ambazo ni Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15
huku kambi ya Temeke ni wagonjwa 9.
Aliendelea
kufafanua kuwa wagonjwa wengi wamekuwa
wakitoka katika maeneo mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni
maeneo ya
makumbusho,kimara,Tandale,Manzese,Saranga,Magomeni,Mwananyamala,kibamba,kigogo,Goba,Burahati,Kinondoni
na Kijitonyama.
Manispaa ya Ilala
ni Buguruni,Majohe,Chanika,Ilala sharif shambana Tabata huku Katika Manispaa ya
Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa Azizi Ally,Keko na Yombo
Vituka.
Alisema
Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na
kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15
wamehifadhiwa kwenye kambi ya Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.
Waziri huyo
wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua tahdhari pamoja
na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa mazingira,kuchemsha
maji ya kunywa,kunawa mikono kwa sabuni
kabla na baada ya kula chakula,kuepuka kusalimiana kwa kushikana
mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo vimeandaliwa
kwenye mazingira safi na salama.
Naye Mwakilishi Mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora amesema kuwa
lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa kemikali maalumu na
kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji au kuchemsha maji.
Aidha aliongeza
kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti kushugulikia
upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazigira katika maeneo husika
nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya pekee bali ni ushirikiano na Wadau
wengine ikiwemo sekta ya Uchukuzi,Mawasiliano,Maji na Elimu.
Katika hatua
nyingine Wizara ya Afya imetoa namba za simu ya mkononi kwa wananchi ambazo ni 0767300234
ambapo zitatumika kuwasiliana moja kwa moja na mganga mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam ili kupata maelekezo ya kitabibu mara baada ya kuhisi dalili za
maambuki ya ugonjwa huo.
MWISHO
CHANZO WIZARA
YA AFYA
MWANDISHI
MUSA AUGUSTINE



































